Mtoto wa darasa la pili katika shule ya Msingi Ifuwa wilaya ya Kilolo John Msasamila akiwa na mzigo wa fimbo ambao mwanafunzi huyo alikuwa ameagizwa na mwalimu wake kwa ajili ya kuwaadhibia wale wanaokiuka maadili ya shule hiyo,hapa naweza kusema elimu ya viboko
Wednesday, September 30, 2009
Monday, September 28, 2009
VIONGOZI WA KITAIFA WAKIDUMISHA UTALII ..............
Hapa lazima nikifaidi hiki chakula cha kiasili
Clement Sanga na Suleiman Boki ( kushoto) wakifanya mashambulizi katika chakula cha asili leo
KURUDI MWANZA HAPA
MAONYESHO YA WIKI YA UTALII YAPUOZA ......
Chui akiwa amelala kwa zaidi ya siku tatu sasa na kufanya maonyesho ya wiki ya utalii upande wa wanyama kuwakwaza wengi hata baadhi kutoa maneno ya kejeli
'Mambo ya dolla haya 'pia hii ni huduma kwa watalii mkoani Iringa
Askari wa wanyamapori wakifungua milango ili kuruhusu watu kuona vyema wanyama wawili waliofikishwa uwanjani hapo
Sokwe
wananchi kiduchu wakishangaa wanyama katika uwanja wa maonyesho ya utalii
''Hata maonyesho yenyewe hayajapendeza kivile mbona simba mwenyewe hayupo "ukitaka kurudi mwanzo bonyeza hapa
Thursday, September 24, 2009
MICHEZO YA UTOTONI YAWEZA KUTOA MWANGA WA MAISHA YA UKUBWANI...
Mtoto Barack Godwin akichezea mafano wa gari leo ,picha hii inatukumbusha michezo yetu ya utotoni na wapo baadhi yetu ambao kutokana na michezo ya utotoni leo wameweza kufanya kweli ila wapo pia michezo hii ya utotoni kwao haijatoa mwelekeo bora wa kimaisha,Je? unakumbuka ni mchezo gani uliopenda kucheza ukiwa mtoto ? na kazi unayofanya inahusiana na mchezo huo?
Wednesday, September 23, 2009
POLISI IRINGA WACHACHAMAA NI BAADA YA BOSS WA SUMRY KUNUSURIKA KWENDA JELA ,BOSS WA HEKIMA NAYE CHUPU CHUPU KWENDA JELA.............
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Mnubi akionyesha picha ya mabasi ya kampuni ya Hekima ambayo bosi wake amehukumiwa kwenda jela miezi nane kwa kushindwa kuajiri madereva wawili
Na Francis Godwin,Iringa
MAHAKAMA ya hakimu mfawidhi wa wilaya ya Iringa imemhukumu kifungo cha miezi 18 jela mkurugenzi wa wa kampuni ya mabasi ya Hekima Joel Panja wa Dar es Salaam kwa kosa la kushindwa kuajiri madereva wawili katika basi lake kama sheria ya mamlaka ya leseni na usafirishaji majini na nchi kavu (SUMATRA) inavyoagiza.
Mkurugurunzi huyo ambaye alifikishwa mbele ya hakimu wa Mahakama hiyo Selfu Kulita alikili kosa lake na kuiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kwa kuwa ni kosa lake la kwanza .
Akisoma shitaka hilo mbele ya mahakama hiyo juzi mwendesha mashtaka wa polisi Inspekta Aseri Mwampamba alisema pamoja na sheria ya Sumatra namba k/f 29 cha sheria ya usafirishaji ambavyo vinaenda kwa pamoja na k/f 17 (1) na (2) cha sheria hiyo ya Sumatra ya mwaka 2007 kuwataka wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuajiri madereva wawili katika mabasi hayo mkurugenzi huyo wa Hekima amepuuza na kuruhusu basi lake kuendeshwa na dereva mmoja kutoka Dar e Salaam kwenda Tunduma mkoani Mbeya.
Alisema kuwa kutokana na msako mkali unaoendelea kufanywa na askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Iringa chini ya mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Mnudi ,askari hao walifanikiwakukamata basi lenye namba za usajali T 400 AVU Scania likendeshwa na dereva mmoja Fortunatus John .
Alisema kuwa basi hilo lilikamawa katika eneo la Check point ya Igumbilo mjini Iringa julai 17 mwaka huu majira ya mchana .
Hata hivyo mkurugenzi huyo baada ya kusomewa shitaka aliloshitakiwa na SUMATRA alikiri kosa lake na kuhukumiwa kwenda jela miezi hiyo 18 jela kabla ya kuiomba mahakama hiyo kujmpunguzia adhabu hiyo ya kufungwa jela.
Kutokana na kuwa ni kosa lake la kwanza na kutokuwa na usumbufu katika kupinga kosa lake hilo ,Mahakama hiyo ilimpunguzia adhabu na kujmtaka kulipa kiasi cha shilingi 300,000 adhabu ambayo aliitekeleza na kunusurika kwenda jela.
Hivi karibuni kurugenzi wa mabasi ya Sumry pia alihukumiwa kwenda jela miaka miwili ama kulipa faini shilingi 500,000 kwa kosa kama hilo katika mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa Iringa hivyo kufanya idadi ya wakurugenzi waliofikishwa mahakamani hadi sasa mkoani hapa kufikia wawili .
MWISHO

Monday, September 21, 2009
KIJANA ANAYE VUMA KTK FANI YA UTANGAZAJI....................
Subscribe to:
Posts (Atom)