Diwani wa kata ya Mseke Iringa Aldo Mwihava ambaye kwa sasa ni mlemavu wa maisha baada ya kukatwa miguu yote akiwa na Rais Jakaya Kikwete nyumbani kwake Mseke jana
Thursday, October 29, 2009
RAIS JAKAYA KIKWETE AMJULIA HALI DIWANI ALIYEKATWA MIGUU IRINGA
Diwani wa kata ya Mseke Iringa Aldo Mwihava ambaye kwa sasa ni mlemavu wa maisha baada ya kukatwa miguu yote akiwa na Rais Jakaya Kikwete nyumbani kwake Mseke jana
Wednesday, October 21, 2009
HOFU YAPUNGUA KWA WANAFUNZI IDODI SEKONDARI
Monday, October 19, 2009
BREAKING NEWSsssssssssssssssss DINI YA AJABU IRINGA YASABABISHA MWANDISHI HUYU KUFARIKI DUNIA..........
Thursday, October 15, 2009
SERIKALI YAMWAGA PONGEZI KWA CHUO CHA TUMAINI IRINGA
Prof.John Shao akizungumza katika uzindunzi wa warsha ya maendeleo ya biashara na ujasiliamali iliyoandaliwa na chuo kikuu kishiriki cha Tumaini Iringa leo
Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI) Aggrey Mwanri (kulia) akimpongeza mratibu wa warsha ya maendeleo ya biashara na ujasiliamali chuo kikuu cha Tumaini Dr Bukaza Chachage leo chuoni hapo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz akimkaribisha mgeni rasimi Naibu waziri wa TAMISEMI
Naibu waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri (wa nne kushoto) akiwa na viongozi wa chuo kikuu cha Tumaini Iringa pamoja na viongozi wa chama na serikali na washiriki wa warsha hiyo leo
Soma habari hii hapa
Saturday, October 10, 2009
WANAFUNZI WAKWEPA MASOMO WAUZA KUNI.......
Wanafunzi wa shule za msingi Idofi na saja wilaya ya Njombe wakitafuta wateja wa kuni mjini Makambako umbali wa Km zaidi ya 20 kutoka kijijini kwao, kuni ambazo wamekuwa wakiza kwa mzigo sh.500 hadi 800 imeelezwa kuwa idadi ya wanafunzi kukwepa vipindi na kufanya biashara ya kuni imekuwa kubwa katika kata ya saja makambako
Thursday, October 8, 2009
BREAKING NEWSsssssssssssssssss MOTO MWINGINE IDODI SEKONDARI
Huku Taifa likiwa katika maombolezo ya vifo vya wanafunzi 12 wa kike katika shule ya sekondari Idodi waliokufa moto na kuendelea kuuguza majeruhi 23 wa ajali hiyo ya moto baada ya bweni hili kuteketea kwa moto hivi karibuni moto ambao chanzo chake ni mshumaa, wanafunzi wa kiume katika shule hiyo leo wamenusurika kuteketea kwa moto baada ya moto kuibuka ghafla katika moja kati ya mabweni ya muda yanayotumiwa na wavulana hao kwa sasa .
Taarifa za kuaminika zilizothibitishwa na viongozi wa serikali ya kijiji cha Idodi na shule hiyo zinadai kuwa chanzo cha moto huu bado hakijafahamika japo moto huo ulianza kuwaka kutoka ndani ya sa nduku la mwanafunzi mmoja wa kiume bwenini humo .
Hata hivyo moto huo haujaleta maafa yoyote baada ya kuzimwa mapema.
Kwa habari zaidi juu ya tukio hili endelea kutembelea blog hii napenda kukutakia usiku mwema.
Monday, October 5, 2009
SHERIA ZA MIPANGO MIJI IRINGA VINAVYOCHANGIA UBOVU WA MJI
Sheria ngumu ya mipango miji katika Manispaa ya Iringa ambayo imekuwa ikizuia wananchi kufanya matengenezo ya nyumba zao hadi pale wanapoomba kibali cha kujenga nyumba za ghorofa imezidi kuuchakaza mji wa Iringa zaidi ,pichani ni moja ya nyumba ambayo ipo mjini Iringa na bado watu wanaishi ila kuta zake zinataka kuanguka na hivyo kushikiliwa na nguzo na kama sheria hiyo isigekuwepo yawezekana kabisa nyumba hii ingefanyiwa marekebisho
Thursday, October 1, 2009
IDODI SASA NI FURAHA TUPU.........................
IDODI SEKONDARI FURAHA TELE LEO..............
Wanafunzi wanaobaki katika shule ya sekondari Idodi wakitoa burudani ya ngoma kwa wa nafunzi wa kidato cha nne wakati wa sherehe za kuwaaga leo
Hii ni familia ya Lukuvi
Hatuamini kama leo tumefikia kikomo hapa Idodi sekondari
Mwalimu Conso Lukuvi akimvisha Levina Lukuvi taji baada ya kuhitimu elimu ya Sekondari Idodi ,wanafunzi hao wanataraji kuanza mitihani yao ya mwisho jumatatu hivyo blog hii inaendelea kuwaombea heri katika mitihani yao,
Usikose kupata makala ya Idodi sekondari katika gazeti la Tanzania daima
Kama unataka kurudi mwanzo bonyeza hapa
Subscribe to:
Posts (Atom)