Waandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima kutoka Pwani, Arusha na Morogoro wakimpa pole mmoja kati ya wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro leo ,waandishi hao ambao ni wanaharakati wa masuala ya kijinsia wamefika hapo kwa ufadhili wa GEMSAT na TMF na wapo mkoani Morogoro kwa mafunzo ya siku tatu ambayo yanamalizika kesho
Friday, November 27, 2009
WAANDISHI GAZETI TANZANIA DAIMA WAONYESHA HURUMA KWA WAGONJWA...................
Waandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima kutoka Pwani, Arusha na Morogoro wakimpa pole mmoja kati ya wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro leo ,waandishi hao ambao ni wanaharakati wa masuala ya kijinsia wamefika hapo kwa ufadhili wa GEMSAT na TMF na wapo mkoani Morogoro kwa mafunzo ya siku tatu ambayo yanamalizika kesho
Thursday, November 26, 2009
Thursday, November 19, 2009
DEREVA AFUTIWA LESENI KWA UZEMBE ..................
Thursday, November 12, 2009
SUMRY HIGH CLASS KWA USAFIRI RAHA NA SALAMA TANZANIA........
Ni usafiri wa uhakika safi na salama kwa safari yako
Kwa mikoa ya Dar es Salaam ,Iringa, Mbeya ,Ruvuma,Rukwa Arusha n.k Safiri na Sumry pekee
Huduma bora kwa kila mmoja na kila mkoa
Madereva wenye uzoefu mkubwa katika taaluma ya udereva nchini
Siti zake ni tofauti na mabasi mengine abiria mmoja kila siti na wawili kila upande tofauti na mabasi lori ambayo siti 3 hadi 4 kwa kila upande
Huduma ya Video hupunguza umbali wa safari
Monday, November 9, 2009
WALIMU IRINGA WAKIGOMEA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA
Na Francis Godwin,Iringa
PAMOJA na Rais wa chama cha walimu nchini (CWT) Gratian Mukoba kutangaza mgomo wa walimu nchini nzima kuanzia leo (jumatatu) kwa lengo la kuishinikiza serikali kuwalipa madeni ya walimu,walimu mkoani Iringa wameonyesha kukigomea chama hicho baada ya kugoma kushiriki mgomo huo na badala yake kuendelea na kazi kama kawaida Tanzania Daima limebaini .
Uchunguzi wa kina uliofanywa na mwanadishi wa habari hizi katika shule mbali mbali za sekondari na zile za msingi mkoani Iringa ,umebaini kuwepo kwa upuuziaji mkubwa wa agizo hilo la Rais wa walimu nchini baada ya walimu hao kugoma kushiriki mgomo bila kuwa na agizo lolote la maandishi kutoka Taifa .
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya walimu wa shule za msingi na zile za sekondari mkoani Iringa walisema kuwa wazo la Rais wao la kutaka walimu wote kugoma ni zuri ila bao wanaona Rais huyo (Mukoba) anaendesha chama hicho kisiasa baada ya kuonekana kulichukulia suala hilo kama utani kwa kuwaagiza walimu kuanza mgomo bila kutoa barua yoyote kwa walimu hao.
Mwalimu Juma Sanga na Anna Joseph walisema kuwa hatua ya serikali kuendelea kuchelewesha kulipa madai ya walimu ni kilio cha walimu wengi na wote wanaodai wangependa kuigomea serikali ila kutokana na kiongozi wao huyo kuishia kutoa mkauli za mezani dhidi ya suala hilo ndio sababu ya wao kupuuza kauli zake na kuamua kuendelea na kazi kama kawaida.
Alisema mwalimu Sanga kuwa Rais Mukoba alipaswa kutoa barua yenye maelekezo ya aina ya mgomo kwa vyama vya walimu wilaya na mikoa ili vyama hivyo viweze kuwasiliana na wakuu wa shule husika kwa ajili ya kuanza mgomo huo ila sio kutangaza kupitia vyombo vya habari huku akijua wazi kuna vingozi ambao wanaweza kufikisha maagizo hayo kabla ya vyombo vya habari.
Hata hivyo walisema kuwa suala la mgomo kwao ni zuri sana ila bado wanamshauri Rais wao huyo kuwa makini anapotoa maagizo ya mgomo ikiwa ni pamoja na kuangalia muda husika na mambo yaliyopo mbele yao walimu na watoto wao.
Kwani alisema kipindi hiki ni cha kufunga mwaka ambapo wanafunzi wapo katika mitihani mbali mbali hivyo hatua ya walimu kugoma ni kuendelea kuyafanya matokeo ya watoto kuyumba na shule kushuka kitaaluma.
"Rais wetu yeye amekuwa akishinda ofisini ila sisi tumekuwa tukishinda mashuleni .....sasa kama wanafunzi watafanya vibaya na serikali ikatulipa madai yetu yote ....walimu wakuu wa shule husika ndio ambao watatakiwa kutoa maelezo kwanini shule vimefanya vibaya na sio yeye kama Rais wetu"
Pia waliutaka uongozi wa CWT Tanzania kukutana na serikali ili kuweza kulizungumza kwa kina suala hilo badala ya kila wakati Rais wao huyo kuendelea kutoa vitisho dhidi ya serikali bila kutekeleza .
Kwa upande wake mwalimu Joseph alisema kuwa Rais wao huyo kabla yakutangaza mgomo anapaswa kutoa maelekezo ya aina ya mgomo na pia mwisho na mgomo huo na hatua zitakazochukuliwa na CWT mwisho wa mgomo kama serikali itakuwa haijawalipa madai yao.
Hata hivyo kwa upande wao viogoza wa CWT mkoa wa Iringa walipotafutwa na mwandishi wa habari hizi jana ili kuelezea sababu za walimu kutoshiriki mgomo huo kama ilivyotangazwa na Rais wao ,ofisi za chama hizo muda wote zilikuwa zimefungwa huku baadhi ya watumishi watumishi wa jengo la TUGHE mkoa wa Iringa lililopo eneo la Pawaga Road wakimtaka mwandishi kuwasiliana na katibu wa CWT Manispaa ya Iringa Peter Mvili ambaye hata hivyo simu yake haikuweza kupatikana.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule za msingi na Sekondari mjini Iringa wamewapongeza walimu mkoani Iringa kutoshiriki mgomo huo .
Wazazi hao walisema kulikuwa na nafasi kubwa kwa viongozi hao kufanya majadiliano na serikali kabla ya kuingia katika mgomo huo ambao madhara yake ni makubwa kwa Taifa .
MWISHO

Sunday, November 8, 2009
RADIO EBONY FM WALETA TEKNOLOJIA MPYA YA JUKWAA IRINGA...................
Jukwaa la kisasa lisilo adui wa mazingira linalomilikiwa na radio Ebony Fm linavyovutia maonyesho mkoani Iringa
Jukwaa pekee ni kivutio tosha katika onyesho la wahapa hapa hivyo hapa naweza kusema hata kama kungekuwa na kiingilio cha watu kufika kushangaa jukwaaa basi yawezekana wengi wangejitokeza kulipia
Tuesday, November 3, 2009
HALI YA MAZINGIRA JIJINI DAR ES SALAAM BADO MBAYA..................
Subscribe to:
Posts (Atom)