AMANI YETU TUSIIVURUGE WATANZANIA

AMANI  YETU TUSIIVURUGE  WATANZANIA

POLISI JAMII NA ULINZI SHIRIKISHI AMANI NA UTULIVU VITATAWALA DAIMA TANZANIA

Tuesday, February 23, 2010

WALIOANZA KUJIPANDA KATIKA MAJIMBO MAPYA IRINGA WAUMBUKA,

WAJUMBE wa baraza la ushauri ya mkoa (RCC) mkoani Iringa washindwa kuridhia mapendekezo mapya ya majimbo ya uchaguzi yaliyopendekezwa na halmashauri za wilaya baada ya kukosa sifa zilizotolewa na tume ya uchaguzi ili jimbo liweze kugawanywa.

Pamoja na kuonyesha kuyatosa mapendekezo hayo ya halmashauri bado wilaya ya Njombe kuna uwezekano wa kupata jimbo jipya katika mji wa Makambako baada ya wilaya hiyo kuwa na mchakato wa kuubariki mji wa Makambako kuwa mji rasmi wajumbe wameridhia hilo.

Wakijadili katika kikao cha dharula baraza la uhauri la mkoa (RCC) leo kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni kilimo chini ya mwenyekiti wake mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz .

Wajumbe hao walishindwa kutetea hoja ya kwanini majimbo ya uchaguzi yaongezwe katika wilaya zao pamoja na kukosa sifa za tume zilizotolewa kwa mikoa yote hapa nchini baada ya baadhi ya mikoa kuwepo kwa taarifa ya kuchukua kazi ya tume ya uchaguzi kwa kujitangazia mapya kinyume na utaratibu.


Mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazin Mzee Jackson Makwete na mbunge wa jimbo la Kilolo Prof.Peter Msolla ndio wabunge pekee waliofika katika kikao hicho nyeti kati ya wabunge 13 wa majimbo 11 na wawili wa viti maalum mkoa wa Iringa.

Akichangia hoja ya kuongeza majimbo katika wilaya ya Njombe mbunge Makwete alisema kuwa ni vyema busara zikatumika katika kujadili suala hilo ili wilaya ya Njombe ikubaliwe kuongezewa jimbo moja zaidi ombi ambalo liliungwa mkono kwa kukubali mji wa Makambako kupendekezwa kuwa jimbo .

Mwenyekiti wa kikao hicho mkuu wa mkoa wa Iringa ambaye ni mbunge wa jimbo la Lindi mjini aliwataka wajumbe kupiga kura wanaotaka Makambako kuwa jimbo na wale wanaopinga pendekezo hilo ambapo wajumbe wote waliunga mkono baada ya kuwepo kwa hoja hiyo nyeti mbele ya Makambako kuwa mji.

Awali wilaya zaidi ya tatu ndani ya mkoa wa Iringa zilikuwa katika mchakato wa kupendekeza ongezeko la majimbo ya uchaguzi kwa madai ya ukubwa wa majimbo hayo na hali ya kijografia katika wilaya sababu ambayo haijaweza kuendana na sifa za tume .

Wilaya zilizokuwa katika mchakato wa mapendekezo ya majimbo mapya ni pamoja na Makete yenye jimbo moja ilipendekezwa kuwe na majimbo mawili ,Njombe yenye Majimbo tatu ilipendekezwa kuwe na majimbo manne ,Ludewa yenye jimbo moja ilitaka kuongeza jimbo la pili na kama Kilolo huku wilaya ya Mufindi ilikuwa ikitaka kuongeza jimbo la tatu kutoka majimbo mawili ya sasa.

Moja ya sifa kubwa iliyokwamisha halmashauri kukosa sifa za kupitishiwa mapendekezo yake ya kugawa majimbo ya uchaguzi ni ile ya idadi ya watu ambapo tume inataka ili jimbo liweze kuwa jimbo lazima liwe na idadi ya watu zaidi ya 200,000 jambo ambalo kwa halmahauri hizo hazijaweza kufikisha zaidi ya kuwa nusu ya idadi hiyo pamoja na sababu nyingine nyingi ambazo zimo katika barua ya tume kwa mikoa yote.

Kabla ya tume kupiga marufuku zoezi la mikoa kutangaza majimbo ya uchaguzi katika mkoa wa Iringa baadhi ya makanda wa CCM wanaotaka kuwania ubunge katika majimbo mbali mbali walianza kujitangazia kuwa wanakusudia kugombea katika majimbo mapya ambayo hata hivyo tume ilikuwa haijataganza zaidi ya kuwepo kwa mapendekezo katika halmashauri pekee.

Thursday, February 18, 2010

RAIS KIKWETE YUPO NCHINI UTURUKI KWA ZIARA YA KIKAZI......













Rais wa Uturuki Abdullah Gul akiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania wakikagua gwaride nchi ya viwanja vya IKULU ya nchini ya Uturuki jana asubuhi,
hongera mdau Freddy Maro kwa kutuhabarisha zaidi

Tuesday, February 16, 2010

MKAPA ADANGANYWA KILOLO,DC ASEMA HALI SHWARI JAPO SI SHWARI................


PAMOJA na wakazi wa kijiji cha Kihesa mgagao katika wilaya ya Kilolo kulalamika kwa uongozi wa wilaya hiyo kuhusu mgogoro kati yao na kampuni ya New Forest inayojihusha na upandaji miti katika eneo hilo kwa kufyaka mazao yao na kupanda miti taarifa ya wilaya kwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa imeonyesha kuficha ukweli kuhusu hali ya usalama katika wilaya hiyo.

Katika taarifa hiyo iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Dr .Athuman Mfutakamba imeelezwa kutokuwepo kwa hali ya migogoro katika wilaya hiyo huku uchunguzi wa mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com umebaini kuwepo kwa migogoro katika wilaya hiyo .


Na kutoka na migogoro hiyo hali ya kisiasa katika wilaya hiyo inaweza kuwa tata na kwa chama cha mapinduzi (CCM) kupata ushindi katika uchaguzi mkuu mwaka huu katika kijiji cha Kihesa mgagao kutokana na mgogoro huo wa ardhi kati yao na New Forest na ule wa gereza la Kihesa Mgagao ambalo wananchi wamekuwa wakilitaka kuondoka katika eneo hilo na majengo yatumiwe kwa matumizi ya shule ya sekondari.


Mkuu wa wilaya ya Kilolo katika taarifa yake kwa Rais Mkapa alisema kuwa hali ya kisiasa katika katika wilaya hiyo ipo vizuri na wananchi wanaendelea na shughuli zao mbali mbali za maendeleo kwa ufanisi huku wakulima na wafugaji wakiendelea na shughuli zao bila kuwepo mitafaruku.


Katika ukrasa wa kwanza wa taarifa hiyo ya wilaya ya Kilolo iliyosomwa na mkuu wa wilaya hiyo Dr Athuman Rashid Mfutakamba inaeleza kuwa hali ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo kuwa hali usalama kwa ujumla ni shwari ,huku ikieleza kuwa matukio ya migogoro inayohusisha makundi ya kidini ,kisiasa ua wakulima na wafugaji kwa kipindi hiki haipo huku mtandao huu ukiwa na taarifa chungu mzima za malalamiko ya wananchi huku baadhi yao wakitishia kuandamana kupinga mwekezaji wa NEW FOREST na gereza la Kihesa Mgagao kuondolewa katika kijiji hicho baada ya wafungwa kudaiwa kutumika kunyanyasa wananchi.


Kuhusu hali ya kisiasa alisema kuwa CCM imeendelea kufanya vyema japo chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kimeendelea ndicho kilichoweza kushika nafasi ya pili katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana kwa kupata nafasi 33 sawa na asilimia 1.3 katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa huku CCM ikipata nafasi 2581 sawa na asilimia 98.7 kati ya nafasi zote 2614 zilizokuwa zikigombewa .

Huku chama cha wananchi (CUF) na vyama vingine katika wilaya hiyo havikuweza kuambulia chochote .

Alisema jumla ya vijiji 32 kati ya 105 ndivyo vilivyofanya uchaguzi huku vijiji 73 havikufanya uchaguzi na kukiwezesha chama tawala kupita bila kupingwa katika uchaguzi huo.

Wakati huo huo wilaya ya Kilolo imempongeza Mkapa kwa jitihada zake kubwa za mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia taasisi yake ya Benjamini Wiliam H.I.V/AIDS Foundation kwa kwa kuiwezesha wilaya hiyo kuopata watumishi katika hospitali teule ya Ilula.

Ziara ya Mkapa katika mkoa wa Iringa imeweza kuvuta umati mkubwa wa wananchi wakiwemo wagonjwa katika hospitali ya teule ya wilaya ya Kilolo Ilula ambao jana waliweza kuacha vitanda vyao na kukaa nje ya jengo la hospitali hiyo wakimsubiri kiongozi huyo mstaafu ambaye alikuwa akikagua majengo ya hospitali hiyo.

Mbali ya wagonjwa hao pia umati mkubwa wa wananchi katika mji wa Iringa na maeneo mbali mbali ambayo msafara wake ulipita walilazimika kusitisha shughuli zao huku barabara zikifungwa kwamuda kwa ajili ya kuupungia mikono msafara wake huku baadhi yao hasa wagonjwa katika hospitali ya Ilula wakimtaka kurudi kugombea tena nafasi ya Urais katika uchaguzi huu.

Kwa upande wake Rais Mkapa pamoja na kupokea taarifa hiyo pia ameweza kueleza sababu za yeye kutozungumza na wanahabari katika mambo mbali mbali na kupelekea waandishi kumzushia kuwa anawakwepa.

Mkapa amesema kuwa lengo lake si kuwakwepa wanahabari bali ametingwa sana na majukumu ya kitaifa na kimataifa katika kushughulikia masuala ya UKIMWI kupitia taasisi yake hiyo .

“Hawa waandishi wamekuwa wakiandika kuwa mimi nawakwepa ila ukweli nina mambo mengi sana na siwakwepi wanahabari.....mimi bado wananchi wananipenda sana hebu tazameni leo umati uliojitokeza na hakuna hata mtu mmoja aliyenizomea”

Undani wa habari hii soma gazeti la Tanzania Daima ama gazeti la Msemakweli jumapili

Saturday, February 13, 2010

BARABARA YA TANZAM YASAIDIA KUKUZA UCHUMI KWA TAIFA YAACHA MAAMBUKIZI YA UKIMWI IRINGA .....


Mwenyekiti wa mtaa wa Ndiuka 'A'Siwema Ally ( kushoto) akiwa na mjumbe wa mtaa huo Conjeta Kalolo wakionyesha sehemu ya makaburi ya ukoo katika eneo hilo la Ndiuka ambalo vifo vya UKIMWI vipo juu
BARABARA kuu ya Tanzania ,Zambia na Msumbiji (TANZAM ) ambayo imepita katikati ya miji ya mkoa wa Iringa ni barabara iliyosaidia kukua kwa maendeleo ya kiuchumi katika mikoa ya kusini huku ikitajwa kuwa chanzo cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI katika maeneo yanayopitiwa na barabara hiyo.


Hakuna asiyetambua kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI katika mkoa wa Iringa ambao ni mkoa wa kwanza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya UKIMWI ya asilimia zaidi ya 15 sasa .


Zipo faida nyingi za kiuchumi ambazo zisingekuwepo ama zingekuwepo kwa hali ya chini zaidi kama barabara hii isingekuwepo katika mkoa wa Iringa .


Uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandao huu kupitia ufadhili wa TMF chini ya asasi ya jinsia na nyombo vya habari kusini mwa Afrika ( GEMSAT) tawi la Tanzania katika maeneo hayo ya kando kando ya barabara hiyo ya TANZAM umebaini kuwepo kwa kasi kubwa ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI yanayochangiwa na barabara hiyo.


Wafanyabiashara wa eneo la Ndiuka katika manispaa ya Iringa na wale wa Ipogolo , Ilula na Ruaha mbuyuni wilaya ya Kilolo wanasema kuwa uwepo na uboreshaji wa barabara katika mkoa wa Iringa umeendelea kukuza uchumi wa maeneo hayo na yale ya mikoa jirani na Iringa .


Salimini Sanga mkazi wa Ruaha mbuyuni na John Mtitu mkazi wa Ilula wanasema kuwa kwa upande wa wilaya ya Kilolo hasa maeneo hayo ya Ilula na Ruaha Mbuyuni uchumi wa wananchi umekuwa ukitegemea sana abiria wanaotumia barabara hiyo .


Anasema Sanga kuwa toka mwaka jana serikali ya mkoa kupitia wakala wa barabara Tanzania(TANROADs) mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na wafadhili wamekuwa wakifanya matengenezo makubwa ya barabara hiyo ya TANZAM hali iliyopelekea uchumi wa wananchi wa maeneo hayo kuendelea kukua kutokana na wageni kuwa wengi zaidi japo kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI pia imezidi kuongezeka .


Pamoja na kuongezeka kwa kasi ya UKIMWI suala la vijana hao wanaofanya kazi katika kampuni ya barabara na wengine wanaoingia katika maeneo hayo kwa ajili ya kupumzika pia limezidi kuwa kubwa zaidi.


" Kwa ujumla barabara hii ina faida sana katika ukuzaji wa maendeleo ya uchumi kwa wananchi waliopo kando kando ya barabara hii ...ila matatizo makubwa yanayoachwa na wageni ni UKIMWI na mimba zisizo na baba kwa watoto wetu"


Mtitu anasema kuwa kuboreshwa kwa miundo mbinu hiyo ya barabara ni sababu kubwa ya wananchi kuendelea kuwa na uchumi mzuri ukilinganisha na mikoa ambayo haifikiki kutokana na ubovu wa barabara zake.


Hata hivyo anasema kuwa kwa upande wa wilaya ya Kilolo hasa katika maeneo hayo ya Ilula na Ruaha mbuyuni uwepo wa barabara hiyo mbali ya kuchangia kukua kwa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja ila bado biashara za ngono zimeendelea kuwa juu zaidi na wageni wengi wamekuwa wakipenda kulala katika maeneo hayo kwa ajili ya kufanya biashara za ngono na kuwashawishi mabinti wa shule kufanya nao ngono kwa ujira wa shilingi 2000 na 5000.



"Sehemu kubwa ya hawa mabinti wa Ruaha Mbuyuni na Ilula wamekuwa wakiambukizwa virusi vya UKIMWI kutokana na tamaa ya fedha inayotokana na kipato duni .....kwani sehemu kubwa wanaojituma katika kufanya kazi ya kuuza bidhaa barabarani ni wanawake watu wazima ila mabinti wengi wanauza miili yao kwa wageni "Yapo baadhi ya maeneo ambayo biashara hii ya ngono kwa wageni imekuwa ya wazi wazi mfano Ilula na Ruaha mbuyuni pamoja na Ndiuka na ukitazama maeneo hayo ndio yenye uchumi mzuri ila kasi ya maambukizi ya UKIMWI pia ipo juu.Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ndiuka 'A' Siwema Ally na mwenyekiti wa mtaa wa Ndiuka 'C' Yustina Sanga wanasema kuwa pamoja na mitaa maeneo mengi yanayopitiwa na barabara hiyo kuwa na uchumi mzuri katika mtaa huo hali ya wananchi wake kiuchumi ni nduni zaidi kutokana na mtaa mzima kuwa na wanaume wanne pekee wenye ajira za kuaminika huku sehemu kubwa ya wakazi wa mtaa huo ni yatima,wajane na wazee.Siwema anasema kuwa sababu ya mtaa huo kuwa nyuma kimaendeleo ni kuktokana na upanuzi wa barabara hiyo ambao umepelekea baadhi ya maeneo ya biashara kuvunjwa na wananchi waliokuwa wakitegemea kupata kipato chao katika maeneo hayo kurudi nyuma kiuchumi .Anasema kuwa suala hilo la kuwaondoa wafanyabiashara katika maeneo ya pembezoni mwa barabara hiyo ndiko kumechangia kwa kiasi baadhi ya mabinti wamitaa mingine ya kata ya Ruaha kujiingiza katika biashara ya ngono kama njia ya kutafuta maisha .Aidha anasema kuwa barabara hiyo imekuwa kitega uchumi kikubwa kwao siku za nyuma kabla ya wafanyabiashara kuvunjiwa maduka yao kwa ajili ya kupisha upanuzi wabarabara.Anasema kuwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI yamezidi kuwa juu na kufanya baadhi ya kaya kuongozwa na watoto ama wazee kutokana na vijana kufa kwa UKIMWI.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Ndiuka 'C' Sanga anasema kuwa kuna haja ya serikali ya Manispaa ya Iringa kuweka mpango kabambe wa kuboresha eneo la Ndiuka kwa kushirikiana na kampuni ya barabara ili maeneo ya biashara kando kando ya barabara hiyo kuwepo.

Mmoja kati ya mabinti wanaoishi na virusi vya UKIMWI katika eneo hilo ambao (majina yao yamehifadhiwa ) wanasema kuwa kwa upande wake aliambukizwa virusi vya UKIMWI kwa shilingi 10000 kutoka kwa mfanyabiashara ambaye tayari kwa sasa amekufa .
Anasema kuwa mfanyabiashara huyo kwa muda mwingi alikuwa na mahusiano naye kimapenzi na siku zote alikuwa akitumia kinga ila siku ambayo aliambukizwa VVU alimrubuni kwa kumpa shilingi 500,000 za biashara ili akubali kufanya mapenzi bila kinga.

“Nilikubali kufanya mapenzi bila kinga ila baada ya hapo mwanaume huyo hakuonekana tena ….na kulingana na siku zinavyozidi kwenda ndivyo hali yangu ilizidi kudhoofu ndipo nilipokwenda kupima na kukutwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI”

Anasema binti huyo wa miaka 30 kuwa wakati akiambukizwa UKIMWI alikuwa na miaka 20 na hadi sasa amefikisha miaka 10 akiwa na virusi vya UKIMWI ila huwezi mtofautisha na mtu ambaye haja ambukizwa virusi vya UKIMWI kutokana na kukubali matokeo na kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI.

“ Huyo mwanaume alikuwa na tabia ya kutuchanganya mimi na mwezangu ambaye baada ya kupima na kubaini tumeathirika yeye aliamua kujinyonga kwa kunywa sumu …ila mimi niliamua kuendelea kutumia dawa”

Binti huyo anasema kuwa wapo baadhi ya mabinti wenzake zaidi ya 20 katika eneo hilo la Ndiuka ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI ila wamekuwa wakiendelea na vitendo vya ngono kama njia ya kujipatia mahitaji yao .

“Mfano hawa wenzangu wanaendelea kujiuza kwa madereva wa malori ambao wamekuwa wakilala hapo ….tena kwa utaalam wangu madereva wa malori walio wengi wamekuwa wakifanya mapenzi bila kinga …hivi UKIMWI utapungua kweli”

Hata hivyo anasema kuwa uwepo wa barabara hiyo ya TANZAM umezidi kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi kwa biashara mbali mbali .

Kwani anasema kwa upande wake kabla ya kuambukizwa VVU alikuwa akinufaika na barabara hiyo ya TANZAM kwa kufanyabiashara za vitenge kutoka Kenya na Zambia ila sasa anajutia maamuzi yake baada ya kuambukizwa ugonjwa wa UKIMWI.

Pia nasema kupitia barabara hiyo ameweza kuwa mfanyabiashara mzuri wa mabinti (madanguro) kwa kuwachukua mabinti mikoa ya Mbeya ,Moshi na Dar es Salaam pamoja na maeneo ya vijijini na kuja kuwaweka katika chumba chake eneo la Ndiuka kwa ajili ya kufanya biashara ya kuuza miili na kuwa kati ya mabinti 40 aliopata kuwaleta Iringa 10 wamekufa kwa UKIMWI na baadhi yao wapo ila hali zao si nzuri.

Afisa biashara katika halmashauri ya manispaa ya Iringa Ipyana Kabuje akielezea kuhusiana na kutolewa kwa wafanyabiashara katika eneo la Ndiuka anasema kuwa suala hilolimefanywa ili kuboresha miundo mbinu na kuwa kuondolewa kwa wafanyabiashara hao hakuchaathiri makusanyo yatokanayo na kodi kwa wafanyabiashara hao.

Hata hivyo anasema kuwa bado barabara hiyo ni bora zaidi katika suala la kukuza uchumi wa Taifa kuliko maduka ya wafanyabiashara hao wa ndiuka na maeneo mengine.

Afisa biashara huyo anasema kuwa jukumu lao ni kuendelea kutoa leseni na kukusanya mapato suala la kuwatafutia maeneo ya kujenga lipo chini ya ofisi ya mipango miji na wao wenyewe wafanyabiashara.

Mratibu wa UKIMWI katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Skitu Mwemsi anasema kuwa pamoja na kuwa tatizo la UKIMWI ni la mkoa mzima wa Iringa ila katika Manispaa ya Iringa hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI yanazidi kutishia usalama wa wakati wa mji huo.

Anasema kuwa kwa sasa takwimu zinaonyesha kati ya watu 10 watano kati yao wameambukizwa VVU na kuwa Manispaa hiyo ina jumla ya asilimia 14.3 ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na watu 2953 ambao wamejitangaza wanatumia dawa za ARVs.

Mratibu huyo anasema kuwa maeneo yanayoongoza kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI ni kata hiyo ya Ruaha ambayo imepitiwa na barabara ya Tanzam , Kihesa ambako inapita barabara ya Dodoma –Iringa ,mwangata na mtwivila.

Hata hivyo anasema kuwa mikakati mbali mbali imewekwa katika kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa jamii.

Anasema kuwa mkatati moja wapo ni ule wa kutoa elimu ya UKIMWI, kuendelea kuwasaidia waathirika namba moja wa janga la UKIMWI ambao ni yatima na wajane.

Hivyo anasema serikali kupitia tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI ( TACAIDs) imeendelea kusaidiana na manispaa ya Iringa kusaidia yatima na elimu kwa umma.

Kwani anasema kati ya kipindi cha mwaka 2007/08 watoto 152 walilipiwa ada ya sekondari kiasi cha shilingi milioni 3.7 na mwaka 2008/09 jumla ya watoto 363 walilipiwa ada ya shilingi milioni 7.7

Wakati vikundi vya waathirika 10 kwa mwaka 2007/08 vilisaidiwa fedha za miradi kiasi cha shilingi milioni 6 na mwaka 2008/09 vikundi 15 vilipewa shilingi milioni 4.7

Pamoja na barabara hiyo ya Tanzam ametaja sababu nyingine zinazochangia maambukizi ya VVU kuongezaka Iringa kuwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Gest bubu ,madanguro ndani ya grosary na vilabu vya pombe za kienyeji pamoja na baadhi ya watu kuonyesha mikanda ya ngono.

Mwandishi wa makala haya ni mwanachama wa GEMSAT – Tanzania anapatikana kwa namba 0754 026 299/0712 750199
www.francisgodwin.blogspot.com au www.matukiodaima.blogspot.com


Mwisho napenda kuushukuru uongozi mzima wa GEMSAT Tanzania kwa kuniwezesha kuufanya utafiti huu juu ya faida ya hasara za barabara hii ya TANZAM pia nawapongeza TMF kwa kuiwezesha GEMSAT

Thursday, February 11, 2010

WANAFUNZI IDODI SEKONDARI WAZIDI KUFUTWA MACHOZI .......

NCHI ya uingereza kupitia mradi wa Secondary Education encourage Development ( SEED) unaoendeshwa katika wilaya ya Iringa vijijini imetoa msaada wa vitanda na vifaa vya shule vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi Iringa waliopatwa na tatizo la bweni lao kuungua moto mwaka jana.

Meneja SEED mkoani Iringa Stephene Likunga akikabidhi msaada huo wa vitanda 18 kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini Fundi Mihayo juzi alisema kuwa msaada huo ni moja kati ya misaada mbali mbali ambayo imekuwa ikitolewa na SEED ndani ya mkoa wa Iringa.

Likungu alisema kuwa pamoja na mradi huo kutoa msaada huo wa vitanda katika shule hiyo ya sekondari Idodi bado imekuwa ikitoa misaada mbali mbali ya kielimu kwa wanafunzi shuleni hapo kabla na baada ya bweni la wanafunzi kuungua moto.

Aliitaja misaada mingine ambayo shule hiyo imepewa kutoka katika mradi huo kuwa ni pamoja na Magodoro 26 masuka 52,sare za wanafunzi 26 ,masanduku ya nguo thamani yake milioni 3 vitu ambavyo vilitolewa kwa ajili ya wanafunzi wanaosomeshwa na SEED .

Akifafanua kuhusiana na misaada hiyo alisema awamu ya kwanza mashuka ,sare za shule na masanduku ya kuwekea nguo vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3 msaada huo uliwalenga wanafunzi waliopatwa na matatizo ya bweni kuungua moto pekee ambao wapo chini ya mradi huo .

Huku awali ya pili SEED imetoka vitanda hivyo 18 vyenye thamani zaidi ya milioni 2 ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wote waliopatwa wa kike shuleni hapo.

Kuhusu wanafunzi wanaosomeshwa na SEED toka ilipoanzishwa mwaka 2004 kuwa ni zaidi ya 70 wakiwemo wanafunzi 40 Idodi sekondari wakati shule ya sekondari Kalenga wapo 30 na kuwa mbali ya uingereza pia nchi mbali mbali duniani zimekuwa zikisaidia wanafunzi hao kupitia mradi wa SEED.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mihayo mbali ya kuupongeza uongozi wa maradi huo pia aliwapongeza wadau wengine ambao wameendelea kutoa misaada yao kwa shule hiyo ya Idodi akiwemo mbunge wa jimbo la Ismani Wiliam Lukuvi ambaye amekuwa akisaidia mara kwa mara shule hiyo.

Mkuu wa shule hiyo Raymond Mlasu alisema kuwa kasi ya ujenzi wa bweni la wasichana ambalo liliungua moto mwaka jana inakwenda vizuri na kuwa wakati wowote kuanzia sasa wanafunzi wataanza kulitumia bweni hilo na kuondoka katika bweni la wavulana ambalo linatumika kwa ajili ya wasichana huku wavulana wakilala katika vyumba vya madarasa.

Mkuu huyo wa shule alisema kuwa mahitaji makubwa kwa sasa katika shule hiyo ni vitanda kwa ajili ya wanafunzi hao na kuwa magodoro yapo ya kutosha baada ya kupokea msaada wa magodoro 500 kutoka CCM makao makuu.

Pia alisema moja kati ya mkakati wa shule hiyo ni kuhakikisha bweni la pili kwa ajili ya wasichana linajengwa shuleni hapo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi kama ilivyokuwa awali.

MWISHO


Meneja SEED mkoani Iringa Stephene Likunga akikabidhi msaada huo wa vitanda 18 kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini Fundi Mihayo alisema kuwa msaada huo ni moja kati ya misaada mbali mbali ambayo imekuwa ikitolewa na SEED ndani ya mkoa wa Iringa.

Likungu alisema kuwa pamoja na mradi huo kutoa msaada huo wa vitanda katika shule hiyo ya sekondari Idodi bado imekuwa ikitoa misaada mbali mbali ya kielimu kwa wanafunzi shuleni hapo kabla na baada ya bweni la wanafunzi kuungua moto.

Aliitaja misaada mingine ambayo shule hiyo imepewa kutoka katika mradi huo kuwa ni pamoja na Magodoro 26 masuka 52,sare za wanafunzi 26 ,masanduku ya nguo thamani yake milioni 3 vitu ambavyo vilitolewa kwa ajili ya wanafunzi wanaosomeshwa na SEED .

Akifafanua kuhusiana na misaada hiyo alisema awamu ya kwanza mashuka ,sare za shule na masanduku ya kuwekea nguo vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3 msaada huo uliwalenga wanafunzi waliopatwa na matatizo ya bweni kuungua moto pekee ambao wapo chini ya mradi huo .

Huku awali ya pili SEED imetoka vitanda hivyo 18 vyenye thamani zaidi ya milioni 2 ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wote waliopatwa wa kike shuleni hapo.

Kuhusu wanafunzi wanaosomeshwa na SEED toka ilipoanzishwa mwaka 2004 kuwa ni zaidi ya 70 wakiwemo wanafunzi 40 Idodi sekondari wakati shule ya sekondari Kalenga wapo 30 na kuwa mbali ya uingereza pia nchi mbali mbali duniani zimekuwa zikisaidia wanafunzi hao kupitia mradi wa SEED.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mihayo mbali ya kuupongeza uongozi wa maradi huo pia aliwapongeza wadau wengine ambao wameendelea kutoa misaada yao kwa shule hiyo ya Idodi akiwemo mbunge wa jimbo la Ismani Wiliam Lukuvi ambaye amekuwa akisaidia mara kwa mara shule hiyo.

Mkuu wa shule hiyo Raymond Mlasu alisema kuwa kasi ya ujenzi wa bweni la wasichana ambalo liliungua moto mwaka jana inakwenda vizuri na kuwa wakati wowote kuanzia sasa wanafunzi wataanza kulitumia bweni hilo na kuondoka katika bweni la wavulana ambalo linatumika kwa ajili ya wasichana huku wavulana wakilala katika vyumba vya madarasa.

Mkuu huyo wa shule alisema kuwa mahitaji makubwa kwa sasa katika shule hiyo ni vitanda kwa ajili ya wanafunzi hao na kuwa magodoro yapo ya kutosha baada ya kupokea msaada wa magodoro 500 kutoka CCM makao makuu.

Pia alisema moja kati ya mkakati wa shule hiyo ni kuhakikisha bweni la pili kwa ajili ya wasichana linajengwa shuleni hapo ili kupunguza msongamano wa wanafunzi kama ilivyokuwa awali.

MWISHO