KIKOSI cha timu ya Radio Ebony Fm Iringa kimeanza maandalizi makubwa ya mchezo wake wa kirafiki kati yake timu ya chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ) pamoja na mashindano ya kombe la Mei Mosi mkoani hapa ( pichani ni mchezaji Francis Godwin ambaye ni mmiliki wa mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com)
Msemaji msaidizi wa timu hiyo ya Ebony Fm Bahati Alex alisema kuwa timu hiyo imeanza maandalizi yake mapema ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake ya michezo miwili ya kirafiki pamoja na mchezo mmoja wa kuwania kombe la mei mosi mkoa wa Iringa.
Alex alisema kuwa DSJ wapo mbioni kuja mkoani Iringa kwa ziara ya kimasomo na katika ziara yao katika kituo hicho cha Radio pia watapata kuchezo mchezo mmoja wa kirafiki kama njia ya kudumisha mahusiano zaidi .
Hivyo mbali ya kuwapongeza wanafunzi hao wa chuo hicho cha habari kwa kufanya ziara ndani ya mkoa wa Iringa bado alisema uamuzi wao wa kuomba mchezo wa kirafiki ni moja ya changamoto kubwa kwa wadau wa soka ndani ya mkoa katika kufufua soka la Iringa.
Hata hivyo alisema pamoja na mchezo huo kati ya Radio Ebony Fm na DSJ pia alisema mchezo mwingine kama huo wa kirafiki utachezwa mjini Mafinga na timu ya watuma salam mkoa wa Iringa.
Alisema baada ya michezo hiyo miwili kikosi chake kitaendelea na mazoezi ya kawaida kwa ajili ya maandalizi ya kombe la Mei mosi mkoa wa Iringa.
Pamoja kuwataka wadau wa soka ndani ya mkoa kuendelea kuelekeza nguvu zao kwa timu changa ili kama njia ya kuibua vipaji vya wachezaji bado alisema kuwa moja kati ya mikakati ya timu hiyo ni kuendelea kuhamasisha soka zaidi ndani ya mkoa .
Alex alisema kuwa kwa upande wa kikosi chake maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya michezo hiyo miwili ya kirafiki na kuwa hivi sasa kikosi hicho kimekuwa kikijinoa katika uwanja wa chuo cha ualimu Mkwawa mjini hapa.
MWISHO