Thursday, May 20, 2010
Friday, May 7, 2010
UTANDAWAZI WAZIDI KUKUA .........
Tuesday, May 4, 2010
NAIBU WAZIRI DK AISHA KIGODA APONGEZA HOTUBA YA RAIS KIKWETE DHIDI YA MGOMO WA WAFANYAKAZI
HUKU hotuba ya Rais Jakaya kikwete aliyoitoa jana wakati akilihutubia Taifa kupitia wazee wa jijini Dar es Salaam ikionekana moto mkali kwa wafanyakazi na hata kuwagawa wafanyakazi hapa nchini ,naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii jana ametumia jukwaa la maadhimisho ya siku ya albino duniani mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda kumpongeza Rais Kikwete kwa hotuba nzuri.
Dk Kigoda ambaye ni waziri wa kwanza katika baraza la mawaziri la serikali ya awamu ya nne kujitokeza mbele ya hadhara kumpongeza Rais Kikwete kwa hotuba yake hiyo ,ametoa pongezi hizo leo kabla ya kumkaribisha waziri mkuu Pinda kuwahutubia wakazi wa mkoa wa Iringa katika maadhimisho ya siku ya albino duniani maadhimisho yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya bustani ya manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa akiwa kama waziri anampongeza sana Rais Kikwete kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa dhidi ya chama cha wafanyakazi hapa nchini ambacho kimekuwa kikitaka kuitisha mgomo wa wafanyakazi nchi nzima kuanzia kesho
Hata hivyo alisema mgomo si njia ya mapatano na kuwa ni vyema wafanyakazi ambao wanataka kuendelea na kazi zao kutii kauli ya Rais Kikwete na sio kuwasikiliza viongozi wao ambao wanaweza kuwapotezea ajira zao.
Waziri huyo alisema serikali iliyopo madarakani imekuwa ikisikia kilio cha wananchi wake na kufanyia kazi kulingana na uwezo wake na kuwa si vyema kwa wafanyakani kushiriki mgomo huo.
Pamoja na waziri huyo pia baadhi ya wafanyakazi wa sekta mbali mbali za serikali katika mkoa wa Iringa ambao hawakupenda kutaja majina yao wamesema hawapo tayari kupoteza ajira zao kwa kushiriki mgomo huo.
Hivyo walisema watakuwa tayari kugoma iwapo Rais wa chama cha wafanyakazi atawaleza makubaliano sahihi kati yake na serikali juu ya vima vya chini vya mishahara kabla ya wao kuendelea kulumbana na serikali.
Hata hivyo walisema bado kuna haja ya watanzania kuungana na kufanya mgomo wa pamoja kupinga ongezeko wa bidhaa ambalo limeendelea kuongezeka kama wakati hasa baada ya serikali kutangaza nyongeza ya mishahara.
"Sisi tunadhani wakati umefika wa wananchi wote bila kujali kazi zetu kufanya mgomo wa pamoja na kupinga ongezeko la bidhaa na kupanda kwa gharama za maisha kila mwaka huku maisha yetu kiuchumi yakiendelea kuyumba...hivi inakuweje kila serikali inapopandisha mishahara bidhaa sokoni pia zinapanda na kodi za nyumba juu"walihoji wafanyakazi hao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa Iringa Beny Kapwani alisema kuwa hotuba ya Rais Kikwete imejaa vitisho na kuwa hakutegemea kama serikali ingefikia hatua ya kuwatisha wafanyakazi kiasi hicho.
Kwani alisema kuwa suala la mgomo ni haki ya wafanyakazi na ipo katika sheria za kazi hivyo ilipendeza serikali kuwaacha wafanyakazi kutumia haki yao ya msingi ya kugoma bila kutishwa.
MWISHO
Sunday, May 2, 2010
MAADHIMISHO YA SIKU YA MAALBINO KUFANYIKA IRINGA KITAIFA
Subscribe to:
Posts (Atom)