AMANI YETU TUSIIVURUGE WATANZANIA

AMANI  YETU TUSIIVURUGE  WATANZANIA

POLISI JAMII NA ULINZI SHIRIKISHI AMANI NA UTULIVU VITATAWALA DAIMA TANZANIA

Tuesday, June 29, 2010

WWW.SHWARI.COM SASA IPO HEWANI TEMBELEA

www.shwa.com,www.shwari.com

www.shwari.com, www.shwari.com,www.shwari.com www.shwari.com,www.shwari.com sasa ipo hewani tembelea,mpendwa mdau nimelazimika kupanua wigo zaidi wa mawasiliano

Saturday, June 26, 2010

SOMO LIMEELEWEKA?




















Wauza magazeti Iringa walivyofanikiwa kukomesha tabia ya watu kugeuza meza za kuuzia magazeti maktaba



Tuesday, June 15, 2010

MWAKALEBELA ASEMA YUPO TAYARI KWA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI.


Fredrick Lameck Mwakalebela wa TFF ametangaza kuwania ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) jimbo linaloongozwa na wake Monica Mbega (CCM).

Monica Mbega ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amekuwa Mbunge wa wa kuchaguluiwa Jimbo la Iringa Mjini kwa awamu ya pili mfululizo hivi sasa na kati ya mwaka 1995 na 2000 alikuwa mbmunge wa viti maalumu.


Akitangaza nia yake hiyo mbele ya waandishi wa habari wa nyumbani kwake Wilolesi mjini hapa leo, Mwakalebela ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Michezo ya VANNEDRICK (T) Ltd alisema anataka kutumia uzoefu alioupata kwenye medani ya soka kuwatumikia wananchi wa jimbo la Iringa.


Mwakalebela aliyezaliwa miaka 40 iliyopita, alisema ni haki yake kikatiba kuchagua na kuchaguliwa kuwaongoza watanzania wenzake bila kujali dini wala makabila yao.


”Nikiwa mwanCCM, mzaliwa wa Iringa ninawiwa kuchangia harakati za maendeleo za jimbo hili kwa kuomba uwakilishi kupitia CCM, na uwezo namaarifa ya kubonyue kitufe kwa ajili ya maendeleo ya jimbo la Iringa ninayo kwa kushirikiana na wakazi wa jimbo la Iringa na wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi” alisema.


Alisema endepo atafanikiwa kuteuliwa na chama hicho kuwa mgombea wake na hatimaye kuwa Mbunge wa jimbo hilo, atatumia maarifa yake yote kuhakikisha jimbo la Iringa linakuwa na vipaumbele vitakavyosaidia kuwaondolea wananchi wake umasikini.


Mwakalebela ambaye ni msomi mwenye shahada ya pili katika masuala ya utawala wa rasilimali watu alisema katika uchaguzi huo kauli mbiu yake itakuwa Maendeleo Kwanza itakayokwenda sambamba na kauli mbiu ya kitaifa ya Kilimo Kwanza.


Alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuvutwa na nia njema ya kuwatumikia watanzania akiwa mbunge wa jimbo la Iringa Mjini ambapo atashirikiana na taasisi mbalimbali, NGOs, CBOs, mashirika ya Umma na binafsi ili kuleta maendeleo jimboni humo.

Alisema kuwa kutokana na kufanya kazi katika sehemu mbalimbali na kuona utendaji wake una mafanikio makubwa, ari hiyo imemvuta zaidi kulitumikia jimbo hilo na kuongeza kuwa uzoefu ambao ameuonesha katika sehemu anazozifanyia amependa kuutumia ili kushirikiana na wananchi wa jimbo la Iringa kuleta maendeleo.

Alisema kuwa ili maendeleo yenye mwelekeo yapatikane jimboni humo makundi yote ya wazee, vijana, akina mama na watoto yanatakiwa yaunganishwe na kiongozi mwenye mtazamo yakinifu utakao kuwa na manufaa kwa jamii nzima bila kubagua kundi fulani, na kuongeza kuwa kwa kulizingatia hilo ameona kuwa anaweza kuwa msaada kwa wana Iringa endapo watamchagua.

Aliongeza kuwa mkoa wa Iringa unazo rasilimali nyingi pia unavivutio vingi vya utalii na kuwa kama vitatangazwa na kukaribisha wawekezaji wengi ambapo kwa kushirikiana na wakulima, wafanyabiashara, vikundi mbalimbali vya wazee, akina mama, walemavu, vijana pamoja na wajasiliamali, wataunganishwa katika mtandao wenye muhimili wenye mafanikio makubwa kwao na kwa taifa.

Alisema atatumia michezo kama 'working tool' yake ya kuyaunganisha makundi yote ya wazee, akina mama, vijana, watoto na watu wa rika zote katika kuhamasisha maendeleo na akongeza kwamba wazee wasiposhirikishwa katika shughuli za kuongoza nchi na kuleta maendeleo mafanikio yatakuwa ni mabaya.

Alisema kuwa uzoefu mkubwa wa kuwaongoza wananchi ameupata katika sehemu mbalimbali ambazo amefanya kazi ikiwa ni pamoja na nchini
Botswana alikokuwa akifanya kazi kama mshauri wa masuala mbalimbali yakiwemo yakiuchumi, kiwanda cha sukari cha Mtibwa na sasa kwa muda wa miaka minne amekuwa ni Katibu wa TFF.

Alisema kuwa uzoefu huo pamoja na kujuana na watu kutoka mashirika, watu pamoja na taasisi mbalimbali hivyo vyote vitamsaidia kuhakikisha wananchi wa jimbo la Iringa wanashirikiana na kuwa kitu kimoja katika kupambana na umasikini ili kuwa na mwelekeo mmoja wa kunyanyua uchumi.

Mwakalebela ametangaza nia yake akiwa pamoja nawanafamilia wenzake ambapo baba yake Mzee Wilfred Makalebela alisema ametoa baraka zote kwa mwanae katika nia yake ya kugombea ubunge ili ashirikiane na wananchi wa jimbo la Iringa kuleta maendeleo endelevu.


Alisema kuwa amepata elimu katika sekondari ya Highlands kidato cha kwanza hadi Nne na sekondari ya Tosamaganga kidato cha tano hadi sita na baada ya kumaliza shahada yake katika Chuo Kikuu cha Mzumbe alifundisha sekondari ya Ufundi ya Ruaha na kwenda kufanya kazi Botswana kwa miaka sita.

Mwisho;

Saturday, June 12, 2010

SIRI YA LUKUVI KUENDELEA KUSHINDA JIMBONI YAFAHAMIKA


MBUNGE wa jimbo la Ismani na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Wiliam Vangimembe Lukuvi ni mbunge wa chama cha mapinduzi (CCM) aliyemkimbiza mwenyekiti cha chama cha Demokrasia(Chadema) mkoa wa Iringa Bw.Beny Mwigongo Kapwani kuendelea kugombea ubunge katika jimbo la Ismani kutokana na kazi kubwa utekelezaji wa Ilani ya CCM iliyofanywa na mbunge huyo jimboni kwake .

Mhe.Lukuvi ni mmoja kati ya wakuu wa mikoa wa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amepata kuzitumikia vema kofia mbili ya ukuu wa mkoa na ubunge kwa wakati mmoja jambo ambalo wapinzani wamekuwa wakipinga mbunge kuteuliwa nafasi uwaziri ,unaibu waziri ama ukuu wa mkoa eti kwa madai ya kushindwa kuwatumikia vizuri wananchi waliomchagua japo kwa mbunge Lukuvi ameweza kupingana na wapinzani hao kwa kuonyesha uwajibikaji wa hali ya juu.

Katika mahojiano maalum na mtandao wa
www.francisgodwin.blogspot.com Bw kapwani anasema kuwa amelazimika kutogombea tena jimbo hilo la Ismani na sasa atagombea jimbo la Iringa mjini katika uchaguzi utakaofanyika octoba mwaka huu.

Pamoja na wachambuzi wa mambo ya kisiasa ndani ya jimbo la Ismani na mkoa wa Iringa wakiwemo wanachama wa chadema wenyewe kudai kuwa Bw.kapwani ameamua kujitoa kugombea kutokana na kukosa kura mwaka 2005 alipojitokeza kwa mara ya kwanza kupambana na Lukuvi na kuambulia patupu ila yeye mwenyewe amedai kuwa jimbo hilo si sehemu ambayo anaishi na kujitokeza kwake mwaka 2005 ilikuwa kuvunja rekodi ya Lukuvi kuendelea kupita bila kupingwa na si vinginevyo.

“Mimi Jimbo la Ismani sigombee tena kwa sasa nagombea Iringa mjini kwa Mhe. Monica Ngenzi Mbega…wewe mwenyewe unajua kuwa mimi naisha hapa mjini… ila juu ya nani atagombea Ismani na Lukuvi itajulikana ila sio mimi “

Kujitoa kwa mwenyekiti huyo wa Chadema hakuwashangazi sana wana CCM kutokana na nguvu ya kiasiasa aliyonayo Mhe.Lukuvi katika jimbo hilo na si nguvu ya jukwani pekee lah hasha bali ni nguvu ya kusukuma mbele gurudumu la kimaendeleo katika jimbo hilo kiasi cha kupongezwa na kila mkazi wa jimbo hilo bila kujali itikadi za vyama vya siasa.

Huku wengi wakiendelea kumfananisha Mhe.Lukuvi na chifu katika jimbo lake kwa kazi kubwa ya kimaendeleo ambayo amekuwa akiifanya ikiwa ni pamoja na kutimiza ahadi na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kama ambavyo alivyoahidi na jinsi ambavyo CCM katika Ilani hiyo ilivyoahidi .

Pia uwajibikaji mzuri wa viongozi hawa wa kuteuliwa na mheshimiwa Rais Kikwete ni heshima kubwa kwa serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Kikwete ila pia ni jambo la kujipongeza kwa wananchi wa majimbo husika hasa kufanikisha kuchagua chaguo jema kwa maana ya mwakilishi wao mbunge ambaye anatazamwa na Taifa zima ,ikumbukwe kuwa tunao wakuu wa mimkoa zaidi ya wanne ambao ni wabunge wa majimbo ambao majimbo yao hata hivyo yanafanya vizuri wakuu hao mbali ya Mhe.Lukuvi ambaye mkoa wa Dar es Salaam umeendelea kupata maendeleo makubwa hasa katika idara ya ulinzi, usafiri kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla na uboreshaji wa mgambo kwa kuwaondoa mgambo wanyanyasaji maarufu kwa jina la (Mumbamba ama Mungiki ) ,yupo mkuu wa Kilimanjaro Mhe.Monica Ngezi Mbega ambaye ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini , Mhe.Mohamed Abdulaziz mkuu wa Iringa na mbunge wa jimbo la Lindi mjini na wengine wengi ila wapo mawaziri na manaibu waziri ambao pamoja na kupewa jukumu la kutumikia Taifa zima ila katika majimbo yao waliowengi mambo yanakwenda vuzuri mfano waziri mkuu Mhe.Mizengo Pinda .

Katika kuuthibitishia umma na kuonyesha kuwa Rais Kikwete hakukosea kuwateua wabunge kushika nafasi nyingine zikiwemo za ukuu wa mikoa mbunge wa jimbo la Ismani mkoani Iringa Mhe.Lukuvi sana sema kuwa katika jimbo lake lenye tarafa tatu kulikuwa na hadi kubwa sita ambazo alipata kuahidi yeye kama mbunge pamoja na zile zilizomo kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005-2010.
Ahadi ya Tarafa ya Idodi;
Akizitaja ahadi hizo kwa kila tarafa na jinsi zilivyotekelezwa kuwa ni pamoja na kutatua kero ya wagonjwa kukosa usafiri katika tarafa ya Idodi kwa kupeleka gari la wagonjwa kituo cha afya Idodi pia ujenzi wa kituo cha afya Mlowa ujenzi ambao unaendelea vizuri sana.

Ahadi ya tarafa ya Ismani ;
Kuwa ilikuwa ni kujenga bweni la wasichana kwa shule ya sekondari na kununua gari ya kubeba wagonjwa kwa kituo cha afya Ismani ,ujenzi wa bweni la wasichana ahadi ambazo zimetekelezwa vizuri japo alisema gari ambalo lilitolewa kwa sasa linasumbua na kuwa jitihada za kutafua jingine zinafanyika .
Ahadi ya tarafa ya Pawaga;

Mhe.Lukuvi anasema katika tarafa hiyo ya Pawaga ahadi kubwa ilikuwa ni ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Pawaga ambalo limejengwa kwa zaidi ya dola 300 za marekani bweni ambalo ni la kisasa zaidi.

Hata hivyo anasema kuwa kufanikiwa kutekelezwa kwa ahadi hizo na shuguli nyingine za kimaendeleo ni kutokana na ushirikiano mzuri wa wananchi wa jimbo hilo kwake , Halmashauri ya wilaya .

Mhe.Lukuvi anasema kuwa pamoja na wanannchi hao bado anawashukuru zaidi wadau mbali mbali wa maendeleo katika jimbo hilo kwa kazi nzuri ya kuchangia kusukuma mbele kasi ya maendeleo jimboni Ismani.

Miongoni mwa wadau ambao mbunge Lukuvi amewataja kwa pongezi ni pamoja na Voda com Foundation, kanisa la Anglikana Tanzania-Dayosisi ya Iringa , kanisa la Roman Katoliki –jimbo la Iringa ,kanisa la kiinjli ya kilutheri Tanzzania (KKKT) dayosisi ya Iringa, benki ya Posta Tanzania, LAPF, NSSF, PSPF, TANAPA, Ubalozi wa Marekani,ubalozi wa Japan , ubalozi wa Korea kusini, mfuko wa wanyamapori ,kampuni ya maziwa ya Asas ya mkoani Iringa chini ya mkurugenzi wake Salim Asas ambaye ni kamanda wa UV-CCM mkoa wa Iringa ,kampuni ya usafirishaji mizigo nje ya Tanzania ya F.M.Abri chini ya kamanda wa vijana UV-CCM Arif Abri,Mbomipa, Mbeya Cement,Twiga Cement, Idara ya wanyama pori ,DAHACO, Zain ,mzee Fliakos na wengine wengi.

Pamoja na wadau hao pia amesema kwa upande wake kama mbunge ameungana nao mkoano kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 541,350,000 fedha kutoka katika mshahara wake kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya jimbo hilo .

Mhe.Lukuvi anasema kuwa fedha hizo ni pamoja na zile za kusaidia kujengwa bweni la wasichana katika shule ya Idodi ambalo liliungua na kusababisha vifo vya wanafunzi zaidi ya 10 katika shule hiyo mapema mwaka jana .

Aidha anampongeza Rais Kikwete kwa kutembelea jimbo la Ismani na Idodi ambapo mbali ya misaada mbali mbali aliyopata kutoa katika jimbo hilo bado aliahidi kufikisha umeme na barabara ya lami Idodi wakati makamu wa Rais Dr.Alli Mohamed Shein pia amekuwa msaada mkubwa katika jimbo hilo kwa kuchangia shule ya msingi Nyang’oro.

Kuhusu hali ya kisiasa jimboni Mhe.Lukuvi amesema kuwa kwake hali ni shwari na kuwa ana uhakika wa kushinda kwa kishindo na kuwa hata madiwani wa CCM pamoja na Rais Kikwete katika jimbo hilo ategemee kupata ushindi wa kimbunga na kuwa wale wanaotaka kugombea nafasi ya urais kwa sasa kupingana na Rais Kikwete wasitegemee chochote na badala yake kuwashauri kuvuta subira.

Pia alisema kwa wana CCM wanaotaka ubunge jimbo hilo kupitia CCM wanakaribishwa japo wanatakiwa kufahamu shughuli za maendeleo zilizofanywa katika jimbo hilo kwa kupita ofisi ya CCM wilaya ama ofisini kwake kupata utekelezaji wa ilani ya CCM
. iwapo wewe ni mbunge,diwani ama ni mgombea wa nafasi yoyote ya kisiasa unataka kuandikiwa makala yako waweza kuwasiliana nami kwa simu 0754 026 299/0712 750199 pia waweza kutembelea mtandao wa
www.francisgodwin.blogspot.com au www.matukiodaima.blogspot.com
MWISHO