AMANI YETU TUSIIVURUGE WATANZANIA

AMANI  YETU TUSIIVURUGE  WATANZANIA

POLISI JAMII NA ULINZI SHIRIKISHI AMANI NA UTULIVU VITATAWALA DAIMA TANZANIA

Monday, July 19, 2010

WALIOCHUKUA FOMU ZA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI NA KALENGA



















Hawa ni wanachama wa CCM Iringa mjini waliochukua fomu leo hii kwa ajili ya kuwania ubunge ,chini ni wana CCM jimbo la Ismani na Kalenga

Monday, July 12, 2010

NI MILIMA PEKEE HAIKUTANI........





Mkurugenzi wa kampuni ya Mwanahali Said Kubene (kulia) akiwa na mkurugenzi wa kampuni ya Free Community Media's Bw Francis Godwin ambaye pia ni mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima na Msemakweli ,wanahabari hawa wamekutana leo katika kijiji cha Mbande wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakatika wote wawili wakiwa katika harakati za kuhudumia wananchi katika tasnia hii ya habari

Sunday, July 11, 2010

BREAKINGNEWzzzzzzzzzzMAJAMBAZI YAVAMIA HOTEL ZA WAJUMBE WA CCM DODOMA














Wakati wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM Taifa asubuhi hii wameanza safari ya kurejea katika mikoa yao ,wajumbe hao wanaondoka Dodoma huku baadhi yao wakiwa wameondoka katika hari ya furaha waliyokuwa nayo baada ya watu zaidi ya 10 wanaodaiwa kuwa ni majambazi kuvamia Hotel zaidi ya 8 na kuwapora wajumbe hao usiku wa kuamkia leo ,habari kamili utaendelea kuipata pindi nitakapo wasiliana na kamanda wa polisi wa mkoa wa Dodoma







































Hapa wajumbe wakitoka katika Hotel hizo baada ya kuporwa mali zao Ingiahapa

BREAKINGNEZzzzzzz NI DR. BILAL MGOMBEA MWENZA ,BOSS DODOMA HOTEL NUSURU ACHAPWE NA WATEJA





Rais Jakaya mrisho Kikwete amemteua aliyekuwa mgombea Urais Zanzibar Dk Billa kuwa mgombea mwenza wake bara,Dr Bilali katika mchakato wa urais Zanzibar alipata kura 53 huku Dr.Shein akipata kura 117 wakati Nahodha akipata kura 33 ambapo JK amesema wote bado ni hitaji kubwa kwa serikali ya bara na SMZ

wakati huo huo taarifa kutoka Dodoma Hotel zinadai kuwa boss wa Hotel huyo nusuru achezee kichapo na wateja baada ya kubadili Stesheni ya TV wakati JK akitaka kumtangaza Dr.Bilal waunguja wamjia juu arudisha stesheni hiyo ,

Pongezi mtandao huu na ule wa www.shwari.com kwa uongozi wa Collau Investment Co.Ltd kwa kunifadhili kurusha matangazo yao ya mkutano mkuu wa CCM moja kwa moja kutoka Dodoma Hotel shukrani za pekee kwa Bw Thadey na Bi Scolla kwa uzalendo waliouonyesha kwangu toka siku ya kwanza juzi hadi usiku huu ninapo maliza shughuli hii nzito kwa wageni msisahau kutembelea eneo la Dodoma Hotel kwa huduma ya Intarnet Cafe ni mabingwa na ukiwa hapo hakuna usumbufu wowote kama ulivyopata kuungana nami toka Dodoma chini ya cafe hiyo kwaherini Dodoma
bofya hapa

WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WAANZA KUPIGA KURA ZA SIRI KUMTHIBITISHA MGOMBEA URAIS BARA DR.JK















BOFYA

WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WAANZA KUPIGA KURA ZA SIRI KUMTHIBITISHA MGOMBEA URAIS BARA DR.JK















BOFYA

WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WAANZA KUPIGA KURA ZA SIRI KUMTHIBITISHA MGOMBEA URAIS BARA DR.JK

Saturday, July 10, 2010

NIPO 'LIVE" MKUTANO MKUU WA CCM DODOMA LEO














Wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kutoka mkoa wa Iringa wakiwa ndani ya Kizota Dodoma
BOFYA

Friday, July 9, 2010

DODOMA HAPATOSHI











Hawa ni wahudumu wa huduma ya Intenet Dodoma Hotel











Mzee Mbigili wa Iringa ambaye alipata kupigwa na walinzi wa Rais Mwinyi kwa kosa la kufungua mlango wa gari la kiongozi huyo bila taratibu wakati Mbigili akiwa Katibu tarafa Iringa mjini na kuishia kusema kazi ya chama ,hapa akichagua nguo ya CCM Dodoma

















Mdau Frank Mbunda (kushoto) akiwa na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Makete Osumnd Kapinga (katikati) mjini Dodoma leo jioni ,taarifa kutokandani ya Sekretariet ya CCM zinadai kuwa tayari panga limepita huku wanachama zaidi ya watano wakienguliwa na Dr Alli Shein ,Dr.Mohamed Bilali na waziri Kiongozi wa SMZ Shams Vuai Nahodha wakipitishwa katika mchakato huo Bofya hapa

Monday, July 5, 2010

FILIKUNJOMBE AKABIDHIWA UBUNGE LUDEWA KABLA YA BUNGE KUVUNJWA...


KAMANDA wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Ludewa Deo Filikunjombe amechangia shilingi milioni 5 na wazee pamoja na baadhi ya wana chama wa cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa mkoani Iringa kwa ajili ya kuchukua fomu ya ubunge na kampeni zake.

Wana CCM hao wamemchangia kamanda huyo jana mjini Ludewa wakati akitangaza nia ya kugombea ubunge himbo hilo linaloongozwa na mbunge wake wa sasa Prof.Raphael Mwalyosi .

Wazee hao wakiongozwa na wabunge wastaafu wa jimbo hilo Peter Simalenga na Matias Kihaule walimkabidhi kamanda huyo wa vijana hundi ya fedha hizo katika mkutano wa hadhara wa kamanda huyo kutangaza nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo hilo.

Akisoma risala ya wazee wa CCM katika wilaya hiyo mbunge Kihaule alisema kuwa wao kama wazee na ni wabunge wastaafu wa jimbo hilo wamechukizwa na hatua ya mbunge wao huyo kuacha vikao vya bunge na kushinda akizunguka jimboni huku akitambua kufanya hivyo ni kuwakosea haki wananchi wa jimbo hilo ambao walipata kumchagua.

Hata hivyo alisema hatua ya mbunge huyo kudanganya baadhi ya mambo ya kimaendeleo kuwa ameyafanya yeye likiwemo la ujenzi wa Mahakama ya wilaya ambayo ujenzi wake ulianza mwaka 2003 kabla ya kuingia madarakani ni moja ya mambo ambayo wameamua kufanya mabadiliko ya haraka ili kumpata mbunge ambaye atawasaidia wananchi na kupelekea bungeni mawazo ya wananchi na si mawazo yake mwenyewe.

Mzee Kihaule alimshauri mbunge Mwalyosi kuachana na siasa na badala yake kuitumia taaluma yake ya uprofesa kwa kwenda kufundisha katika vyuo badala ya kutumikia nafasi asiyoiweza.

Akielezea kuhusu kamanda huyo wa vijana alisema kuwa wao kama wazee wameona ni mkomavu wa kifikra na mtazamo,ni kijana mwenye adabu na utii wako kwa jamii bila kujali rika, jinsia wala eneo mtu anakotoka.

Pia ana ushirikiano mzuri na wananchi na ni mtu kujichanganya na jamii na kujali shida na matatizo yetu, mpaka kujali namna na kutafuta mbinu za kusaidia kutatua matatizo ya wananchi tofauti na mbunge wao Prof.Mwalyosi

“Hakika yapo mambo mengi uliyoyafanya ya kuyaeleza hapa, lakini kwa kusudio la ombi letu kwako, Sisi wazee tumeshawishika kwa pamoja kukuomba wewe mwanetu Deo Filikunjombe ugombee ubunge mwaka huu 2010”

Hata hivyo walisema kwa vile utaratibu wa kisiasa kikatiba ndani ya CCM unawataka viongozi wapatikane kwa kupigiwa kura na kufuata taratibu nyingine ila kama sio hivyo walikuwa wapo tayari kumsimika rasmi ubunge kabla ya kupigiwa kura ama hata kabla ya bunge kuvunjwa .

unatulazimisha kuwapata viongozi kwa utaratibu wa kupiga kura vinginevyo sisi wazee wako kwa kuzingatia uwezo wako tungekusimika na kukupa uongozi wa jimbo kwa ridhaa yetu moja kwa moja bila hata ya kupiga kura.

“Sisi wazee wako kwa kuzingatia upana na uzito wa jambo hili na gharama zake tumejikakamua kwa hali zetu na kuchangishana kidogo tulicho nacho na tumepata shilingi millioni tano (5,000,000/=) za kuchukulia fomu ambazo leo tunakukabidhi...Pia sisi wazee wako leo tunakuvalisha MGOLOLE na kukukabidhi MKUKI na tunakupatia KIGODA cha kukalia...kama ishara ya mtawala wetu mpya”

Hata hivyo kwa upande wake Filikunjombe aliwapongeza wazee na wana CCM hao kwa hatua yao ya kumwomba agombee ubunge na kumchangia kiasi hicho cha fedha na kuwataka wana CCM kushikamana ili kulifanya jimbo hilo kuendelea kuwa mbele kimaendeleo.

Kamanda huyo wa vijana pia alieleza kusikitishwa kwake na hatua ya mbunge huyo wa sasa Prof.Mwalyosi kumchafua na kuwa amefulia kifedha na kuuza kisima cha mafuta na kuwa mbunge huyo si mkweli hata kidogo na kumwomba kutowachukia wana CCM wanaotaka kuwania nafasi za uongozi katika jimbo hilo.

Wakati huo huo zaidi ya wanachama 20 wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Ludewa walirejesha fomu zao kwa kama njia ya kumuunga mkono kamanda huyo wa vijana kugombea ubunge jimbo hilo.

Picha zaidi utazipata katika mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com leo jioni

Thursday, July 1, 2010

MADEGA ,RIDHIWANI NA MWAMOTO WAMWOMBEA DUA MWAKALEBELA













Mwakalebela akiwa na msafara wake wa wa piki piki walifika kupamba msafara wa JK Dodoma








Mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Bw .Frederick Mwakalebela akiwa na timu ya wapiga debe wa JK mikoa ya Kusini

















John Komba akiteta jambo na katibu mkuu wa TFF na mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini (CCM) Bw Frederick Lameck Mwakalebela mjini Dodoma leo ,nyuma ni wana CCM wengine waliofika kumsindikiza mgombea urais wa CCM Rais Dkt Jakaya Kikwete .









Mwamasishaji wa vijana wa Chipukizi Taifa Esta Bully na mjumbe wa baraza kuu la vijana Taifa Christian Fwalo wakiwa katika picha ya pamoja na mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela katika viwanja vya Ikulu mjini Dodoma .








Rais wa chama cha wachezaji wa Zamani Tanzania (SPUTAZA) na mgombea ubunge jimbo la Kilolo Venance Mwamoto(kushoto) wakipongeza na katibu mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela nje ya jengo la makao makuu ya CCM Dodoma kwa uamuzi wao wa kutaka kugombea ubunge katika jimbo la Iringa mjini na Kilolo








Mjumbe wa baraza kuu la Vijana (UVCCM) Taifa mtoto wa rais Ridhiwani Kikwete (kushoto) na Makamu mwenyekiti wa UVCCM Taifa Beno Malisa wakiwa nje ya jengo la CCM Dodoma ,wakimpongeza katibu mkuu wa TFF Frederick Lameck Mwakalebela kutangaza kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini


RAIS wa chama cha wachezaji wa zamani Tanzania (SPUTAZA) Venance Mwamoto na Rais wa Yanga Imani Madega wamempongeza katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela kwa uamuzi wake wa kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini(CCM)Mbali ya marais hao pia mjumbe wa baraza kuu la vijana Taifa Ridhiwani Kikwete ameungana na viongozi hao kumpongeza Mwakalebela kwa uamuzi wake wa kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini na kuwa kwa upande wake anamtakia ushindi mwema.

Wadau hao wa michezo waliyasema hayo leo mjini Dodoma mara baada ya mgombea urais wa CCM Rais Jakaya Kikwete kumaliza kurejesha fomu yake .

Ridhiwan alisema kuwa akiwa kada wa CCM na mwana michezo amefurahishwa sana kukuta idadi ya wanamichezo wakiendelea kuwania nafasi mbali mbali na kuwa jitihada ambazo zimeonyeshwa katika TFF ndizo ambavyo wanategemea katibu huyo wa TFF Mwakalebela atazionyesha katika kuwaletea maendeleo wana Iringa mjini .

Hivyo alisema kuwa wakazi wa jimbo la Iringa mjini wanayo bahati sana kwa katibu huyo wa TFF kuwa mmoja kati ya wagombea wa ubunge jimbo hilo na kuwa iwapo watashindwa kumchagua watakuwa wamepoteza bahati kubwa ya utendaji wake.

Pamoja na mtoto huyo wa Rais Kikwete kumtakia mafanikio Mwakalebela katika nafasi hiyo anayogombe katika jimbo la Iringa mjini pia chama wa waendesha umoja wa waendesha piki piki mkoa wa Dodoma na Dar es Salaam ambao walifika katika maandamano ya kumsindikiza mgombea huyo wa Urais kurejesha fomu yake ,wameeleza kufurahishwa kwao na hatua ya Mwakalebela kugombea ubunge na kuwa wana imani kubwa jimbo la Iringa mjini limempata mgombea mpenda maendeleo.


katibu wa chama hicho cha waendesha piki piki mkoa wa Dar es Salaam na Dodoma Ramadhan Kaswa alisema kuwa wanaendelea kumwombea dua katibu huyo ili aweze kuchukua ubunge jimbo hilo la Iringa mjini ambalo kwa sasa linaogozwa na mbunge wake Monica Mbega anayekwenda kumaliza muda wake baada ya bunge kuvunjwa.

Huku Rais wa wachezaji wa zamani Tanzania (SPUTAZA) Venance Mwamoto alisema kuwa imani ya watanzania kwa Mwakalebela bado ni kubwa na kuwa iwapo wana Iringa wana taka maendeleo ya kweli ni lazima kuwachagua wagombea wenye uelewa mpana kama katibu huyo.

Mwamoto ambaye pia ni mgombea ubunge wa jimbo la Kilolo alisema kuwa yeye kama mwana michezo anajisikia vizuri zaidi kuona viongozi wakuu wa TFF wanaingia katika bunge na kuwa upo uhakika wa bunge lijalo kuwapata mawaziri na manaibu waziri wenye uelewa mpana wa michezo nchini kama Mwakalebela.

Naye Rais wa Yanga Imani Madega ambaye pia alifika katika hafla hiyo mjini Dodoma alisema kuwa hatua ya Mwakalebela kuwania ubunge ni mafanikio kwa wana michezo nchini na kuwa iwapo atashinda basi wana michezo wategemee makubwa zaidi.

Akizungumza na wanahabari mjini hapa Mwakalebela alisema kuwa anaimani kubwa wana Iringa watampa nafasi hiyo ya kumrithi mbunge wa sasa .Kwani alisema lengo lake ni kutaka kutumia elimu yake na uwezo wa ndani ya nchi na nje ya nchi wa kiutendaji katika kuwatumikia wana Iringa mjini na kulifanya jimbo hilo kuwa jimbo la kipekee katika maendeleo.
picha zaidi jioni ya leo tembelea www.shwari.com na www.francisgodwin.blogspot.com