AMANI YETU TUSIIVURUGE WATANZANIA

AMANI  YETU TUSIIVURUGE  WATANZANIA

POLISI JAMII NA ULINZI SHIRIKISHI AMANI NA UTULIVU VITATAWALA DAIMA TANZANIA

Monday, August 30, 2010

MFANYABIASHARA MAARUFU IRINGA AFUNGWA JELA KWA WIZI WA MAHINDI


Mahakama ya hakimu mkazi wa mkoa wa Iringa imemhukumu kifungo cha mwaka moja jela na faini ya shilingi milioni 1 mfanyabiashara maarufu mjini Makambako wilaya ya Njombe mkoani Iringa Bw Mohamed Khalifa Mnyagani kwa kosa la uchepushaji mahindi ya msaada tani 10.pichani ni kamanda wa Takukuru mkoa wa Iringa Bw Donacian Kessy,habari zaidi soma hapa

Wednesday, August 18, 2010

MONICA MBEGA AJITOKEZA KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE













Monica Mbega akitoka katika ofisi ya msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Iringa kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo hilo leo









Hapa akiingia katika gari tayari kwa safari ya kurudi ofisi za CCM








Monica Mbega akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu leo na kumpongeza Frederick Mwakalebela kwa kuokoa jahazi kuzama








Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa Teresia Mahongo (kushoto) akimkabidhi fomu Monica Mbega











Wapambe wa Mbega wakiwa nje wakisubiri atoke kuchukua fomu .Soma hapa

Tuesday, August 10, 2010

LYANDEMBELA SEKONDARI SASA MAMBO SWARI


WAKATI hali ya utulivu ikionekana kurejea katika shule ya Sekondari ya Lyandembela Ifunda wilaya ya Iringa vijijini baada ya wanafunzi kuendelea na vipindi vya masomo kama kawaida vyombo vya usalama katika mkoa wa Iringa vinamhoji mlinzi wa kanisa la Morovian Ifunda ambaye anadaiwa kuendesha huduma ya kuwatoa mashetani wanafunzi hao huku akiwa si mchungaji wala kiongozi wa kanisa jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.


Pia wanafunzi hao wamepinga mkuu wa shule hiyo aliyesimamishwa kukanyaga ardhi ya shule hiyo kwa ajili ya kwenda kukabidhi mali za shule na kutaka makabidhiano yafanyike nyumbani kwake na sio shuleni hapo.

Mlinzi huyo anayeshikiliwa na jeshi la polisi kwa kujifanya mchungaji ni Ajuaye Golden mzaliwa wa wilaya ya Makete mkoani Iringa.

Hatua hiyo imekuja jana baada ya wanafunzi wa shule hiyo kumtaja mlinzi huyo mbele ya wazazi , viongozi wa elimu na wale wa vyombo vya ulinzi na usalama wilaya kuwa wamekuwa akiwaombea na kutolewa mapepo na mlinzi huyo anayelinda kanisa la Morovian lililopo jirani na shule hiyo.

Akielezea hatua iliyochukuliwa na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa kuhusiana na tatizo hilo kaimu afisa elimu mkoa wa Iringa Euzebio Mtavangu alisema kuwa mbali ya kumwamisha aliyekuwa mkuu wa shule hiyo kwa usalama wake ila bado wanafunzi hao wanatakiwa kuanza masomo mara moja na iwapo watagoma kuingia madarasani basi shule hiyo itafungwa kwa muda usiofahamika.

"Ndugu wazazi na wanafunzi hatua ambayo tumekubaliana kuanzia sasa ni hawa wanafunzi wote kuingia madarasani na kuanza vipindi leo hii(jana) na kama wataendelea kuogopa kuingia madarasani kwa madai kuwa na majini milangoni basi kuanzia sasa wasiingie na warudi nyumbani na sisi tuifunge shule hii...tena kuanzia sasa mwanafunzi atakayeanguka vipindi vitaendelea na mwanafunzi huyo atarejeshwa nyumbani kupumzika "

Hata hivyo alisema kamati ya ulinzi na usalama mkoa chini ya mkuu wa mkoa Mohamed Abdulaziz imeafiki mkuu huyo wa shule kuhamishwa shule kwa ajili ya usalama wake japo serikali haiamini ushirikiana .

"Leo hapa tunamkabidhi kwa muda shule hii rasmi aliyekuwa makamu mkuu wa shule hii ila bado tunaonya wanafunzi na wazizi kujiepusha na manabii wa uongo ambao wanawarubuni wanafunzi kuwa wasisome kwa madai hata kama wakisoma shule hii haitafaulisha milele "

Kuhusu uhaba wa walimu wa baadhi ya masomo katika shule hiyo alisema kuwa ndani ya wiki hii walimu zaidi watakuwa wameongewa katika shule hiyo wakitokea shule ya sekondari Idodi .

Aidha alisema kuwa kwa viongozi wa dini wanaofika katika shule hiyo na shule nyingine kuendesha vipindi vya dini ni vizuri wakazingatia mitaala ya elimu ili kuondokana na uchochezi wa kimaombi kama uliofanywa na mlinzi huyo aliyejifanya ni mchungaji.

Pamoja na afisa elimu huyo kutaka wanafunzi hao kutulia na kuendelea na masomo huku akiwataka kumwacha mwalimu aliyesimamishwa kufika shuleni hapo kufanya mababidhiano ya mali za shule ,bado wanafunzi hao walipinga mwalimu huyo kumwona shuleni hapo na kutaka mali za shule wakabidhiane nyumbani kwake na sio shuleni hapo.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa serikali ya kata ya Ifunda Laurent Kiwovele alisema kuwa hadi sasa wamempiga marufuku mlinzi huyo kuendelea kuendesha kanisa hilo wala wanafunzi kutoka shuleni hapo na kwenda katika kanisa hilo kutolewa mapepo.

"Tumemzuia mlinzi huyo wa kanisa kuendelea kutoa huduma hiyo na tumemkabidhi katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa hatua zaidi kwa kuwa hana sifa za kufanya hivyo na toka alipoanza kutoa mapepo ndipo wanafunzi walipoonyesha kuzidiwa zaidi na mapepo"

Tukio la wanafunzi wa shule hiyo kuanguka lilitokea juzi ambapo zaidi ya wanafunzi 30 na walimu wawili walipoteza fahamu kwa muda kutokana na ugonjwa huo wa kuanguka(mapepo).
MWISHO