
Chama cha ushirika cha kuweka na kukopa cha Faraja Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimetoa msaada wa mahitaji mbali mbali kwa watoto yatima zaidi ya 300 wanaosoma katika shule za msingi wilayani Mufindi.
Meneja mkuu wa Faraja Mafinga Clever Ndanzi alizitaja a shule zilizonufaika na msaada huo kuwa ni pamoja na shule ya mzingi Upendo ,Mkombwe zote na mjini Mafinga na shule ya msingi Mtula na Matanana wilizopo nje ya mji wa Mafinga na kuwa kila shule watoto yatima 75 watapatiwa msaada huo.
Aliitaja misaada ilitolewa na Chama hicho kwa yatima hao ambao ni msaada uliotokana na sehemu ya faida ya mapato ya mwaka kwa chama hicho ,kuwa ni pamoja na sababuni,mafuta ya kupakaa na vifaa mbali mbali vya shule .
Kwani amesema kuwa chama hicho kimekuwa na utaratibu wa kutumia faida yake inayopatikana kwa mwaka kwa jaili ya kuisaidia jamii yenye shida mbali mbali wakiwemo yatima na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na waathirika wa janga la Ukimwi ndani ya wilaya hiyo.
Ndazi alisema kuwa ushirikia huo ulianzishwa mwaka 1999 na wanachama 18 ambapo hadi sasa kuna jumla ya wanachama zaidi ya 650 ambapo jumla ya mikopo iliyotolewa hadi sasa kwa wanachama wake ni zaidi ya shilingi bilioni 1.
Kwa upande wake mwenyekiti wa ushirika huo Macelina Mosha alisema kuwa pamoja na kuwasaidia watoto hao bado jamii ya wilaya ya Mufindi inanalojukumu la kuendelea kuwasaidia watoto yatima huku akiahidi kuwa chama chake kitaendelea kuwasaidia watoto hao kutokana na faida inayopatikana kila mwaka.
Bi Mosha alisema kuwa mikakati na mwelekeo wa chama hicho unataraji kufahamika wazi siku ya jumamosi wiki hii wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama ambapo pia wanachama watapokea taarifa ya mwaka ya chama na kujua makisio na mapato na matumizi ya mwaka 2011.
MWISHO