AMANI YETU TUSIIVURUGE WATANZANIA

AMANI  YETU TUSIIVURUGE  WATANZANIA

POLISI JAMII NA ULINZI SHIRIKISHI AMANI NA UTULIVU VITATAWALA DAIMA TANZANIA

Monday, November 28, 2011

MAHAFALI YA 15 CHUO CHA UFUNDI STADI VETA IRINGA NA CHANGAMOTO ZAKE

MAMLAKA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI

TAARIFA FUPI YA CHUO CHA VETA IRINGA

CHUO CHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI NA HUDUMA IRINGA

Mheshimiwa mgeni rasmi: Mjumbe wa bodi ya VETA Kanda ya Nyanda za juu

Mkurugenzi wa VETA Kanda ya nyanda za juu,
Wakuu wa taasisi mbalimbali,
Waandishi wa habari,
Wageni mbalimbali walio pamoja nasi,
Wafanyakazi wenzangu wote wa VETA
Wahitimu wote,
wanafunzi wote wanaoendelea na mafunzo,
mabibi na mabwana,

Awali ya yote nakushukuru sana wewe binafsi kwa kukubali kushiriki nasi katika Mahafali haya ya 15 ya Chuo chetu.
Aidha niwapongeze kwa dhati kabisa wageni wetu wote kuja kushiriki nasi katika kuwapongeza na hatimaye kuwatunuku Vyeti Wanachuo wetu ambao wamehitimu mafunzo yao.

Mheshimiwa mgeni rasmi,

Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Iringa kinamilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Tanzania (VETA).

Chuo hiki kilifunguliwa rasmi na kuanza utoaji wa Mafunzo mnamo January 1997.

1.Mafunzo yotolewayo
Mheshimiwa mgeni rasmi,

Chuo chetu kinatoa mafunzo ya muda mrefu na mafunzo ya muda mfupi.
· Mafunzo ya muda mrefu yatolewayo hadi sasa ni ya fani mbalimbali kumi na moja (11) kama ifuatavyo:-

1. Umeme wa majumbani
2. Uhazili
3. Useremala
4. Uashi
5. Utengenezaji wa Magari
6. Uungaji vyuma
7. Ukerezaji na Uchongaji Vyuma
8. Upakaji rangi Majengo na Maandishi
9. Ufundi bomba
10. Ushonaji nguo
11. Utayarishaji wa Vyakula

Mafunzo ya muda mfupi
Mheshimiwa mgeni rasmi,

Sambamba na Mafunzo ya muda mrefu Chuo kinatoa pia Mafunzo ya muda mfupi kulingana na mahitaji ya mteja. Zifuatazo ni kozi ambazo Chuo kimeendelea kuzitoa:-
· Udereva
· Kompyuta
· Uhazili

Mheshimiwa Mgeni rasmi,
Chuo kina jumla ya wanafunzi 303 hadi tarehe ya leo (Wasichana 79 Wavulana 224) wasichana asilimia 26.1 Wavulana asilimia 73.9


NA.
FANI
L -I MWAKA WA 1
L-I MWAKA WA 2
L - 2

WAS
WAV
JUML
WAS
WAV
JUMLA
WAS
WAV
JUMLA
JUMLA KUU
1.
USEREMALA



0
09
09
0
16
16
25
2.
UMEME



01
20
21
0
19
19
40
3.
UHAZILI
22
02
24
16
0
16



40
4.
BOMBA



02
13
15
0
07
07
22
5.
UCHONGAJI
V YUMA
01
17
18
0
12
12



30
6.
UUNGAJI VYUMA
01
18
19
0
15
15



34
7.
UASHI



0
08
08
0
15
15
23
8.
UTAYARISHAJI CHAKULA*
16
02
18
-
-
-
-
-
-
18
9.
RANGI NA MAPAMBO
02
11
13
05
08
13
-
-
-
26
10.
USHONAJI NGUO



09
02
11
04
0
04
15
11.
MAGARI
0
18
18
0
12
12



30
JUMLA
42
68
110
33
99
132
04
57
61
303
2.WAHITIMU
Mheshimiwa mgeni rasmi
Katika Mahafali ya leo tunao Vijana 79 (wasichana 20 sawa na asilimia 25.3 na Wavulana 59 sawa na asilimia 74.7
NA.
FANI
WASICHANA
WAVULANA
JUMLA
1.
Uzalishaji Chakula
16
02
18
2
umeme
0
19
19
3
Ushonaji Nguo
04
0
04
4.
Useremala
0
16
16
5.
Bomba
0
07
07
6.
Uashi
0
15
15

Jumla
20
59
79


3. Mafanikio
Mheshimiwa mgeni rasmi,
Katika kutekeleza majukumu yake na malengo mbalimbali Chuo kimepata mafanikio yafuatayo:-
3.1 Kozi fupi
Mwaka huu wa 2011 Chuo kinategemea kutoa jumla ya wahitimu wa kozi fupi zaidi ya 400).
3.2 Kujitangaza
Kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari, Chuo kimekuwa kikiyatangaza mafunzo yake na huduma mbalimbali zinazotolewa hapa,hatimaye kupata mwitikio unaostahili.
3.3 Mafunzo ya Watumishi
Waalimu 05 wamekwenda kuchukua Mafunzo mbalimbali ya muda mrefu. Na Mkutubi 01.
3.4 Huduma mbalimbali:-
Chuo kimeendela kutoa huduma mbalimbali kama
Kantini inavyotoa huduma ya vyakula na vinywaji kwa wateja mbalimbali.
Hostel ya wageni yenye vyumba 20
Kumbi mbalimbali za mikutano na sherehe
3.5 Chuo kimeweza kukamilisha hadi sasa majukumu yake kulingana na mpango kazi.

3.6 Kwa kushirikina na Wanachuo, kazi mbalimbali zilifanyika kwenye karakana, kazi za nje, michezo na shughuli za mazingira zimetekelezwa na zinaendelea kutekelezwa ipasavyo.

3.7 Chuo kimeendelea kushirikina na taasisi mbalimbali ndani na nje ya Iringa katika kuboresha utendaji kazi.


3.8 Mipango yetu mwakani:
Mategemeo ya mwakani ni kupanuwa fani ya utayarishaji wa vyakula kwa kuanzisha idara za
· Front office.
· House keeping.
· Food bevarage and selling.
3.9 Mipango ya baadaye.
Kwa vile eneo la chuo chetu ni Kidogo pengine kuliko vyuo vyote vya VETA Tanzania, chuo kina mpango wa kujenga mabweni eneo la Kitwiru ili kuongeza idadi ya Wanafunzi.

4. Changamoto
Mheshimiwa mgeni rasmi,
Kila penye mafanikio na changamoto zinakuwepo, kwa mfano:-

4.1 Mafunzo kwa vitendo (Field training), ili vijana waweze kuwa mahiri katika fani zao, mafunzo kwa vitendo ni muhimu sana.
Pamoja na jitihada za Chuo za kutafuta sehemu mbalimbali za kufanyia mafunzo hayo: kumekuwepo vikwazo kadhaa kama vile, Wadau wengine kukataa kuwapokea vijana, kwa kudai gharama za mafunzo yao wanapokuwa kwenye sehemu zao.

4.2 Chuo kina uwezo wa kuchukuwa wanafunzi zaidi ya 350 lakini mabweni yaliyopo huchukuwa wanafunzi 106 tu kati ya hao wasichana ni 30 na wavulana ni 76 hivyo kusababisha waombaji wengi kutochukuliwa kujiunga na Chuo.Tumejaribu kutafuta Mabweni ya bei nafuu ndani ya Manispaa ya Iringa lakini tumeshindwa.

4.3 Michezo
Kutokana na eneo la Chuo kuwa dogo, Wanachuo wanapata matatizo ya kushiriki kikamilifu kwenye michezo mbalimbali baada ya masomo.Hata hivyo tunawashukuru jirani zetu wa shule ya Msingi Mlandege ambao wamekuwa wakitusaidia kutatua tatizo hili.

4.4 Maji
Chuo kimekuwa kikikabilina na tatizo la kukatika maji kutoka vyanzo vya JR IRUWASA na hivyo kuathiri mafunzo na utoaji wa huduma nyinginezo za hapa Chuoni.

4.5 Umeme
Chuo kama sehemu ya jamii kimeendelea kupambana na adha ya kukatika mara kwa mara kwa umeme ambao ni nishati muhimu katika kutekeleza majukumu yake kitendo ambacho suluhisho lake ni kuwa na jenereta lenye uwezo mkubwa.
5. Hitimisho

Mheshimiwa mgeni rasmi,
Ninachukua fursa hii, kuwapongeza sana Wanachuo kwa juhudi, usikivu wao na nidhamu katika ufuatiliaji wa mafunzo yao na hivyo kuleta mafanikio makubwa kwao na kwa Chuo chetu.

Tunaowaomba waendelee na ari hiyo ili waweze kuboresha maisha yao huko waendako.

Aidha, tunawaomba wahitimu wetu wawe mabalozi wetu wazuri kuwashauri Vijana wenzao kujiunga na Vyuo mbalimbali vya Mafunzo ya ufundi Stadi, kwani Ufundi ni jibu la haraka katika harakati za kupambana na kutokomeza umaskini hasa pale ambapo kijana ataajiriwa au kujiajiri.

Ahsanteni sana.